Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maisha ya wanawake na watoto milioni 16 kuokolewa

Maisha ya wanawake na watoto milioni 16 kuokolewa

Sambamba na mkutano wa malengo ya maendeleo ya milenia, Umoja wa Mataifa leo umezindua mkakati wa kuokoa maisha ya mamilioni ya wanawake na watoto.

Katika uzinduzi huo mjini New York Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema karne ya 21 lazima iwe na mabadiliko kwa kila mwanamke na kila mtoto.

Uzinduzi huo ambao umehudhuriwa na wakuu wa nchi na wawakilishi wa serikali, sekta binafsi, wahisani, mashirika ya kimataifa, jumuiya za kijamii na mashirika ya utafiti umeanza juhudi za kimataifa za kuokoa maisha ya wanawake na watoto milioni 16, na wadau wamesha ahidi dola bilioni 40 kwa ajili ya afya ya wanawake na watoto.

Jason Nyakundi anaripoti

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)