Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wajadili athari na umuhimu wa kuhifadhi bayo-anuai

UM wajadili athari na umuhimu wa kuhifadhi bayo-anuai

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo limejadili athari na umuhimu wa kuhifadhi bayo-anuai mjini New York kama mchango wao katika mwaka wa kimataifa wa bayo-anuai.

Baraza hilo limesema kuhifadhi viumbe vya dunia na makazi yake na matunda na huduma wanayotoa ni muhimu sana katika maendeleo endelevu na malengo ya maendeleo ya milenia. Baraza hilo limeongeza kuwa mwaka huu sio tuu ni wa kimataifa wa bayo-anuai bali muda wa mwisho kwa ahadi ya jumuiya ya kimataifa ya kuhakikisha imepunguza kiwango cha kupotea kwa bayo-anuai.

Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu Ban Ki-moon sayansi inatuambia kumekuwa na ongezeko la kupotea kwa bayo-anuai na sababu ni rahisi, shughuli za mwanadamu, ikiwa ni pamoja na ukataji miti, kubadili makazi, mmomonyoko wa udongo na mabadiliko ya hali ya hewa. Amesema na waathirika wakubwa ni watu masikini

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ameongeza kuwa wote tunahitaji kuonyesha kwamba kulinda bayo-anuai na mfumo wa maisha kutasaidia kufikia malengo ya maendeleo ya milenia na kudhibiti ongezeko la mabadiliko ya hali ya hewa.