Michezo kusaidia kutekelezwa kwa malengo ya milenia: Ban

21 Septemba 2010

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema kuwa michezo ina wajibu muhimu wa kuitimizwa kwa malengo ya milenia.

Matamshi ya Ban yanajiri wakati viongozi kutoka sehemu mbali, mbali duniani wanapokutana mjini New York kwenye mkutano unaojadili hatua zilizopigwa katika kutimizwa kwa malengo ya milenia yakiwemo ya kuangamiza umaskini, njaa na magonjwa itimiapo mwaka 2015.

Akiongea kando na mkutano huo Ban amesema kuwa jamii ya kimataifa inastahili kutumia mfano wa michezo kama moja ya njia ya kufikia malengo ya milenia. Amesema kuwa kuwepo kwa ushirikiano ni suala muhimu akisema kuwa michezo ni ishara tosha jinsi ushirikiano ulivyo muhimu kwa kutimizwa kwa lengo kwa pamoja.

Ban ameongeza kuwa mamilioni ya watu kote duniani wanashirikia kwenye miradi inayohusiana na michezo sehemu za mashinani ambayo inawasaidia vijana kujizuia na vitendo vikikwemo vya matumizi ya mihadarati na pia kuchangia katika utunzi wa mazingira.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter