Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa IMF asema kundi kubwa la watu duniani litaendelea kutopoa kwenye umaskini

Mkuu wa IMF asema kundi kubwa la watu duniani litaendelea kutopoa kwenye umaskini

Watu zaidi ya millioni 70 duniani kote wanaweza kujikwamua kimaisha na kuondokana na hali ya ufukara, na hii ni kwa mujibu wa fuko la fedha ulimwenguni IMF.

Mkurugenzi Mkuu wa fuko hilo la fedha Dominique Strauss-Kahn amesema kuwa idadi kubwa ya watu duniani wataendelea kuishi maisha ya kiwango cha chini na hii ni kutokana na hali mbaya ya uchumi iliyoshuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni.

Mkwamo wa uchumi ulioanzia katika mataifa yaliyoendelea na baadaye kusambaa katika mataifa kadhaa, kumesababisha kukosekana kwa baadhi ya huduma muhimu ikiwemo kukosekana kwa nishati ya kutosha na kuwepo kwa kitisho cha njaa. IMF inasema watu wengi wataendelea kukosa utengamao wa kiuchumi hadi ifikapo mwaka 2020.

IFM imeonya kuwa kama kutakosekana utashi wa kukabiliana na hali hiyo na kurejesha uwiano wa ukuaji uchumi katika mstari sawio, kunaweza kukatia kikazo kikubwa katika ufikiaji wa malengo ya maendeleo ya mellenia.