Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafuriko yazidi kusambaratisha watu Pakistan:OCHA

Mafuriko yazidi kusambaratisha watu Pakistan:OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema wiki saba baada ya mafuriko nchini Pakistan maelfu ya watu bado hawana makazi hasa katika jimbo la kusini la Sindh.

Kwa mujibu wa Ocha kila siku wanashuhudia watu 20,000 hadi 30,000 wapya wanaokimbia mafuriko. Ziwa Manchar limefurika pia mahali ambako watu wengi walikimbilia kupata hifadhi. Hata hivyo OCHA inasema asilimia 22 ya fedha zilizoombwa Ijumaa iliyopita zimepatikana ambazo ni dola milioni 434 na milioni 53 zinatarajiwa hivi karibuni.

Maradhi ya mlipiko na matatizo ya chakula imeelezwa kuwa bado ni tatizo kwa watu zaidi ya milioni 20 wanaoishi kwa kutegemea msaada hivi sasa. Shirika la mpango wa chakula duniani linasema linafanya kila liwezekanalo kuwasaidia wahitaji. Emilia Casella ni msemaji wa WFP

(SAUTI YA EMILIA CASELLA)