Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LCD's zimepiga hatua katika malengo ya milenia:Ban

LCD's zimepiga hatua katika malengo ya milenia:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema nchi zinazoendelea zimepiga hatua katika moja la malengo muhimu ya maendeleo ya milenia.

Ban ameyasema hayo kwenye mkutano maalumu kuhusu tathimini ya malengo hayo kwa nchi masikini unafanyika sambamba na mkutano wa kimataifa wa malengo ya milenia. Amesema miongoni mwa mafanikio ni katika uandikishaji watoto shule, baadhi ya nchi zimepiga hatua kubwa kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano na wengi wamejitahidi katika kuhakikisha huduma ya maji safi.

Ban amesema mafanikio haya ni hatua kubwa ikizingatiwa yametokea wakati wa migogoro ya kimataifa. Hata hivyo uchumi unaolegalega na malengo ya milenia vinasalia kuwa katika shinikizo kubwa.  Ban ameongeza kuwa nchi zinazoendelea zinasalia kuwa kundi linalokabiliwa na changamoto katika kuhakikisha zinafikia malengo hayo.

Amesema umasikini bado ni mkubwa na zaidi ya nusu ya watu milioni 800 walioko katika nchi masikini wanaishi chini ya msitari wa umasikini. Ni nchi 49 pekee zilizo na umasikini chini ya asilimia 30.