Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chanzo cha kutokuwepo usawa wa kijinsia lazima kishughulikiwe:UM

Chanzo cha kutokuwepo usawa wa kijinsia lazima kishughulikiwe:UM

Afisa wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema sababu ambazo ndio mizizi ya kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia zinahitaji kushughulikiwa

Akizungumza mjini Geneva hii leo naibu mkuu wa haki za binadamu Kyung-wha Kang amesema ni lazima kutazama kwa undani zaidi ya mifumo inayoonekana ya ubaguzi dhidi ya wanawake kama ubakaji na ukatili.

Bi Kang amesema kuna tabia ya kutoa kauali na kuchukua hatua tuu dhidi ya mifumo na dalili za ubaguzi kama ubakaji na dhuluma dhidi ya wanawake kwenye maeneo ya migogoro, ukatili dhidi ya wanawake, mauaji na uhalifu unaofanywa kwa minajili ya kukumbatia mila au dini.

Amesema hili linatia hofu na linahitaji tuchukue hatua, lakini pia tunahitaji kushughulikia kiini cha kutokuwepo usawa jambo ambalo linawarudisha nyuma wanawake na wasichana.