Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya imepiga hatua kufikia malengo ya milenia:Kibaki

Kenya imepiga hatua kufikia malengo ya milenia:Kibaki

Rais Mwai Kibaki wa Kenya amesema nchi yake imepiga hatua kubwa katika kufikia malengo ya amaendeleo ya milenia.

Akizungumza hii kwenye mkutano wa kutathimini hatua zilizopiga kufikia malengo hayo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York amesema ingawa miaka iliyosalia ni mitano tuu kufikia muda wa mwisho ana imani kubwa kuwa Kenya hata kama haitoyafikia yote basi japo nusu yatakuwa yametimizwa.

Akizungumza na mkuu wa Idhaa hii Flora Nducha mara baada ya hotuba yake Rais Kibaki amesema hata hivyo juhudi bado zinahitajika ili kenya kutimiza azma ya malengfo yote manane.

(MAHOJIANO FLORA NA RAIS KIBAKI)