Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rwanda kuwahamisha walioko katika ameneo hatari kimazingira

Rwanda kuwahamisha walioko katika ameneo hatari kimazingira

Rwanda imechukua hatua za kutekeleza mpango wa Umoja wa Maatifa wa utunzaji wa mazingira.

Mpango huo una lengo la kuokoa msitu wa Gishwati na kuzilinda jamii zilizo karibu na sehemu zinazokabiliwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Msitu wa Gashwati ambao awali walikuwa wanaishi sokwe na tumbili kwa sasa umeharibiwa na maporomoko ya ardhi , mafuriko na huduma za wanadamu hali ambayo pia imesababisha maafa na kuharibu makaazi.

Kama moja ya njia ya kuzuia eneo hilo kuathirika na mmomonyoko wa udongo Umoja wa Mataifa una mpango wa kutumia asilimia 43 ya ardhi ya msitu huo kama malisho , kwa upanzi wa matunga na msitu na pia kuulinda msitu huo kutokana na uharibifu wa wanadamu.

Kwa upande wake serikaIi ya Rwanda imetenga jumla ya dola milioni 25 zitazotumika kuwawatafutia makao mapya watu wanaoishi katika maeneo yaliyo hatarini kimazingira kwenda maeneo salama.