Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali Somalia yalaani Al-Shabaab kupiga maruguku misaada

Serikali Somalia yalaani Al-Shabaab kupiga maruguku misaada

Serikali ya Somali imelaani hatua za kundi la wanamgambo la Al- Shabab za kuyaamuru mashirika matatu ya kutoa misaada kusitisha shughuli za utoaji misaada kwa wale wanaoihitaji nchini humo.

Mapema kundi la Al Shabab lilichoma na kupora mashirika kadha ya umoja wa mataifa na mengine ya kimataifa likiwemo shirika la mpango wa chakula duniani WFP. Shughuli za utoaji wa misaada nchini Somali zinatatizwa na ukosefu wa usalama kwa wafanyikazi wa mashirika hayo kutoka kwa kundi la wanamgambo la Al Shabab.

Hatua za Al Shabab zinatajwa kama ukosefu wa heshima dhidi ya raia wa Somalia ambao wamepoteza makwao na kwa ambao sasa wanaishi kama wakimbizi wa ndani ambao wengi wao wanaishi katika hali mbaya ya umaskini kwenye mahema katika maeneo ya kusini na kati kati mwa Somali.

Hatua hizi pia zinalenga kuwanyima wasomali katika maeneo haya kila njia ya kupata usaidizi na kuwalazimisha kulitegemea kundi la Al Shabaab hasa kwenye maeneo masikini