Jumuiya ya kimataifa yaongeza msaada CAR
Jumuiya ya kimataifa imeongeza msaada wake kwa jamuhuri ya afrika ya kati kama msukumo wa kulisaidia taifa kupata amani na kupiga hatua kimaendeleo hasa baada kuonyesha kujitolea kwake katika mpango wa kupatikana kwa amani katika miaka ya hivi majuzi.
Kwa sasa Benki ya Dunia na tume ya amani ya Umoja wa Mataifa wameshirikiana kundaa hafla kubwa kando la mkutanu mkuu wa Umoja wa mataifa wa malengo ya milenia .
Hafla hiyo ina lengo la kuupa nguvu mpango wa amani katika jamhuri ya afrika ya kati pamoja na maendeleo vyote vilivyo ajenda kuu kwenye jamii ya kimataifa.