Ban atoa wito wa hatua za haraka kuisaidia Pakistan
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametaoa wito wa hatua za haraka kuchukuliwa nchini Pakistan baada ya janga la mafuriko yaliyosababisha maafa.
Ban ameyasema hayo kwenye mkutano wa mawaziri ambao pia ulihudhuriwa na waziri wa mambo ya nje wa pakistan Makhdoom Qureshi na wanadiplomasia 25 wa ngazi za juu kujadili janga la mafuriko lililoikumba pakistan alilotaja kuwa gumu zaidi katika historia ya Umoja wa Mataifa.
Akiongea na waandishi wa habari mjini New York Ban amesema kuwa mkutano huo una lengo la kuhakikisha kuwa Pakistan imepata usaidizi wa misaada na ujenzi mpya baada ya watu milioni 20 kuathirika na mafuriko hayo. Mkutano huo unajiri baada ya Umoja wa Mataifa kuitisha msaada wa dola bilioni mbili kutoka kwa wahisani kuwasaidia karibu watu milioni 14 nchini Pakista kwa muda wa miezi 12 ijayo.