Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tukijitolea na kushikana tutaleta amani Somalia:Mahiga

Tukijitolea na kushikana tutaleta amani Somalia:Mahiga

Hatma ya amani ya Somalia hadi sasa bado ni kitendawili japo juhudi kubwa za kitaifa na kimataifa zinafanyika.

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Balozi Augustine Mahiga akiwasilisha ripoti yake kwenye baraza la usalama wiki hii amesema ingawa hali ya usalama na matumaini ya amani ya kudumu yanaonekana kuwa ndoto lakini ndoto hiyo itatimia endapo juhudi za pamoja zitafanyika.

Yaani Umoja wa Mataifa, Somalia yenyewe,na wadau wengine wote. Amezungumza na Flora Nducha kuhusu hali nzima ya nchi hiyo