Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zichukuliwe dhidi ya wabakaji DR Congo:Baraza la usalama

Hatua zichukuliwe dhidi ya wabakaji DR Congo:Baraza la usalama

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limesema linataka hatua zichukuliwe dhidi yanawanaoendesha vitendo vya ubakaji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika taarifa yake kwenye kikako kilichokuwa kkinajadili hali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baraza hilo limepitisha tamko linalomitaka serikali ya Congo kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika na ubakaji wa watu wengi hivi karibuni nchini humo. Ubakaji huo umelaaniwa vikali na Umoja wa Mataifa , mashirika ya kutetea haki za binadamu na jumuiya za kijamii ambapo wote wametaka sheria ichukue mkono wake.

Tangu kuzuka kwa vita nchini humo na hasa katika maeneo ya mashariki mwa Congo, vitendo vya ukatili,unyanyasaji na ubakaji dhidi ya wanawake vimeongezeka na mara nyingi wanaotekeleza vitendo hivyo wamekuwa wakikwepa mkono wa sheria.