Viongozi wa dunia wanajiandaa kutathimini malengo ya milenia Tz imefikia wapi?

Viongozi wa dunia wanajiandaa kutathimini malengo ya milenia Tz imefikia wapi?

Kuanzia Jumatatu ijayo wakuu wa nchi na wawakilishi kutoka wanachama wote 192 wa Umoja wa Mataifa wanakusanyika mjini New York kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Safari hii ni kutathmini hatua zilizopigwa katika mchakato wa kufikia malengo makuu manane ya maendeleo ya milenia ifikapo 2015.

Nchi mbalimbali zimepiga hatua na zingine bado zinasuasua. Je Tanzania iliyoko Afrika mashariki imepiga hatua kiasi gani? Tukianzia na lengo namba moja kutokomeza umasikini na njaa. George Njogopa anatabanaisha katika makala hii kutoka Dar es salaam.