Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 150,000 waathirika na mafuriko nchini Chad

Watu 150,000 waathirika na mafuriko nchini Chad

Mafuriko makubwa katika miaezi miwli iliyopita nchi Chad yamewaathiri watu takriban 150,000 wakiwemo 70,000 ambao ni wakimbizi wa ndani.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Mvua kubwa zinazonenyesha katika eneo la Kusin Mashariki mwa Chad zimeleta athari kubwa kwa kuharibu makambi ya wakimbizi na kuvuruga kabisa mifumo ya miundo mbinu. Sehemu kubwa ya mazao ambayo yalivunwa kwa wingi msimu huu pamoja na mashamba pia yameharibiwa vibaya na mvua hiyo ambayo pia imesababishwa msimu wa kuanza kwa shule ucheleweshwa kwa muda.

Kuna wasiwasi kwamba kutokana na kuharibika kwa mazao mengi huenda eneo hilo likabaliwa na tatizo la njaa.  Watu zaidi 150,000 wamekosa makazi kutokana na nyumba zao kuharibiwa na mvua, na kati yao 4,000 ni wakimbizi. Wataalamu wa afya wametadharisha kuwa eneo hilo huenda likakubwa na magonjwa ya mlipuko.