Skip to main content

Wanaovuka ghuba ya Aden waendelea kuuawa:UNHCR

Wanaovuka ghuba ya Aden waendelea kuuawa:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema limepokea ripoti za mauaji na kuzama kwenye ghuba ya Aden.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka kwa wahamiaji waliowasili Yemen jana raia wa Ethipia alipigwa hadi kufa na kisha kutoswa baharini na watu waliokuwa wakiwasafirisha kiharamu kwa kutumia boti iliyokuwa na wahamiaji na wakimbizi wa Kiafrika wapatao 105 ambao wengi wao ni Waethiopia.