Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa haki za binadamu wahofia ghasia Sudan

Wataalamu wa haki za binadamu wahofia ghasia Sudan

Baraza la haki za binadamu leo limeipitia ripoti ya mtaalamu wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Sudan.

Mtaalamu huyo Mohamed Chande Othman katika ripoti yake ameelezea hofu juu ya utekelezaji wa hukumu ya kifo nchini Sudan, ghasia zinazoendelea nchini humo na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaoambatana na mambo ya uchaguzi Sudan Kusini. Amesema katika eneo hilo la Sudan Kusini kumekuwa na ongezeko la ghasia zinazosababisha kupotea maisha ya watu hususan wanawake na watoto.

Kwa upande wa Darfur bwana Othman amesema kumekuwa na ongezeko la machafuko ya kutumia mtutu wa bunduki na usalama mdogo kutokana na unyang'anyi na vitendo vya utekaji. Naibu waziri wa Marekani Daniel Baer akizungumza mjini Geneva amesema

(SAUTI YA DANIEL BAER)