Ombi la msaada zaidi wa kimataifa kwa Pakistan latolewa

17 Septemba 2010

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limwataka wahisani wa kimataifa kuongeza msaada wa fedha ili kukidhi mahitaji ya haraka wa chakula na ujenzi mpya wa Pakistan.

Josette Sheeran mkurugenzi wa WFP amesema hakuna ambaye angeweza kutabiri ukumbwa na athari za mafuriko ya Pakistan ambako wanawake na watoto wanakabiliwa na hatari ya njaa na utapia mlo. Amesema WFP inahitaji kupanua wigo wa misaada yake nchini humo haraka lakini haitafanikiwa endapo haitakuwa na fedha za kutosha kutekeleza azma hiyo. Shirika hilo linahitaji dola milioni 600 ili kuweza kutoa msaada wa chakula hadi Julai 2011.

Mchana wa leo Umoja wa Mataifa kupitia mwakilishi wake wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA watatoa ombi lingine kwa ajili ya kuongeza msaada na mipango kwa ajili ya Pakistan. Takribani dola zaidi ya bilioni moja zitaombwa ili kukidhi mahitaji ya mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter