Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kimataifa ya amani, kauli mbiu vijana kwa ajili ya amani na maendeleo

Leo ni siku ya kimataifa ya amani, kauli mbiu vijana kwa ajili ya amani na maendeleo

Leo ni siku ya kimataifa ya amani na ujumbe ni kwa vijana kuichagiza na kuidumisha amani kote duniani.

Leo ni siku ya Kimataifa ya amani

(SAUTI YA BAN KI_MOON)

na huyo ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika hafkla maalumu ya kuadhimisha siku hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York akisema leo tunaadhimsha siku ya ya kimataifa ya amani, siku ambayo imetengwa kwa ajili ya kusitisha vita na kupinga machafuko. Ban amesema ndio maana kila mwaka siku ya leo ninapiga kengele ya amani.

Kauli mbiu ya siku ya kimataifa ya amani mwaka huu ni vijana kwa ajili ya amani na maendeleo na Ban ki-moon ametoa wito kwa vijana kote duniani kuchukua msimamo wa amani kwa kuuliza "unafanya nini kwa ajili ya amani?"

Hafla ya siku hii kwenye UImoja wa Mataifa imeambatana na hotuba mbalimbali na majadiliano ambapo wanafunzi 500 wa shule za New york wamejadili sula la amani kwa kuanganishwa kwa njia ya video na wanafunzi wenzao wa Sudan na Liberia.