Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na kufutwa vyama 10 vya siasa Myanmar

Ban asikitishwa na kufutwa vyama 10 vya siasa Myanmar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea masikitiko yake kufuatia kufutwa kwa vyama 10 vya siasa nchini Myanmar ikiwemo chama cha mwanasiasa mashuhuri anayetumikia kifungo gerezani.

Ban amesema amesikitishwa na uamuzi huo uliochukuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na ametoa wito vyama hivyo virejeshewe hadhi yake ili viweze kushiriki kwenye uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka huu.

Mapema mwezi uliopita, Katibu Mkuu huyo ameitaka serikali ya nchi hiyo kuwaachilia huru wafungwa wote wa kisiasa walioko gerezani akiwemo kiongozi wa chama cha NLD na ambaye pia ni mshindi wa tuzo la NOBEL Daw Aung San Suu Kyi. Nchi hiyo inatazamia kufanya uchaguzi wake wa kwanza November 7 mwaka huu baada ya kupita miaka 20.