Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maafisa wa zamani wa Khmer Rouge kupanda kizimbani

Maafisa wa zamani wa Khmer Rouge kupanda kizimbani

Mahakama inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa umewafungulia mashitaka maafisa wanne waliokuwa katika utawala wa zamani wa Khmer Rouge Cambodia.

Watu hao waliokuwa madarakani kati ya mwaka 1975 hadi 1979 wnashitakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo uhalifu dhidi ya ubinadamu, mauji ya kimbari, utesaji na mauaji ya kidini. Aliyekuwa makamu wa kiongozi wa Khmer Rouge lead Pol Pot atapanda kizimbani mwakani pamoja na kiongozi wa zamani wa serikali , na aliyekuwa waziri mkuu wa utawala huo na mkewe.

Inakadiriwa kwamba watu zaidi ya milioni mbili waliuawa Cambodia na 800,000 kati yao kikatili sana wakati utawala wa Khmer Rouge ulipokuwa madarakani.