Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya Niger kupata afueni njaa yaitikisa Chad

Baada ya Niger kupata afueni njaa yaitikisa Chad

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeonya kuwa kiwango cha utapia mlo miongoni mwa watoto nchini Chad kimefikia pabaya.

Mkurugenzi wa WFP Jossete Sheeran amesema hali ya Chad inatia hofu baada ya msimu mbaya wa mvua watoto wengi wameathirika na wanahitaji kuendelea kupata msaada wa chakula na lishe. Mvua kutonyesha ipasavyo mapema mwaka huu imesababisha kuharimika kwa mavuno yote ya 2009 kwenye eneo karibu lote la Sahel na kusababisha njaa kubwa na ongezeko la utapia mlo.

Amesema bei ya chakula nchi humo imepanda sana na hivyo WFP inabidi kuendelea kugawa msaada kwa miezi mingine mitatu. Kila mwaka WFP imekuwa ikilisha watu zaidi ya milioni 90 kutoka nchi 70 duniani.