Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM aelekea Guinea baada ya kuahirishwa uchaguzi

Mwakilishi wa UM aelekea Guinea baada ya kuahirishwa uchaguzi

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Afrika ya Magharibi kesho Ijumaa anaelekea nchini Guinea kujadili namna ya kumaliza tofauti za kisiasa zilizojitokeza.

Bwana Said Djinnit atafanya mazungumzo na wagombea wote wa Urais, maafisa wa tume ya uchaguzi na wanasiasa mashuhuri akiwasihi kuepusha rapsha zozote zinazoweza kujitokeza na kuleta machafuko.

(SAUTI YA SAID DJINNIT)

Hali ya sintofahamu ilizuka baada ya tume ya uchaguzi kutangaza kuahirishwa kwa duru ya pili ya uchaguzi uliokuwa ufanyike Jumapili ijayo. Kwa mujibu wa msemaji wa tume Thiemo Ceydou Bayo uchaguzi umeahirishwa baada ya mazungumzo kati ya waziri mkuu wa mpito na wagombea wawili wa Urais Celleou Dalein Diallo na Apha Conde.