Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi zaidi zahitajika kukomesha machafuko Somalia:Mahiga

Juhudi zaidi zahitajika kukomesha machafuko Somalia:Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Dr Agustine Mahiga amesema mgawanyiko ndani ya serikali ya mpito ya Somalia TFG umetoa mwanya kwa wanamgambo kuongeza mashambulizi dhidi ya serikali, wananchi na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika AMISOM.

Amesema serikali ya mpito itamaliza muda wake Agosti 2011 na kwa kuzingatia makubaliano ya Djibouti ili kuhakikisha amani inarejea na kuundwa kwa serikali ya kudumu kuna masuala muhimu ya kukamilisha kwa Somalia yenyewe na jumuiya ya Kimataifa.

Kwa Somalia amesema lazima kuwe na maridhiano na kukamilisha katiba, lakini pia jumuiya ya kimataifa inapaswa kuongeza juhudi kusaidia AMISOM, kuipa uwezo Somalia kudhibiti Al Shabaab wanaotekeleza mauaji na vitendo vya kigaidi na kubwa zaidi kuwalinda mamilioni ya Raia wanaokufa na kukimbia makazi yao kila siku.