Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ombi la EU lagonga mwamba kwenye baraza kuu la UM

Ombi la EU lagonga mwamba kwenye baraza kuu la UM

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limetofautiana kuhusu hatua iliyopendekezwa na jumuiya ya Umoja wa Ulaya ya kumteua mwakilishi wake kuhutubia baraza hilo.

Katika upigaji wa kura juu ya suala hilo, nchi 76 ziliupinga mswaada huo dhidi ya 71 zilizotaka kuendelea na mchakato wa kupitishwa kwa azimio hilo. Nchi 26 ziliamua kutofungamana na upande wowote.

Umoja wa Ulaya uliwasilisha mapendekezo yake ukitaka kupewa nafasi kwa Rais wa Umoja huo Herman van Rompuy pamoja na mkuu wake wa sera za nje na usalama Catherine Ashton wahutubie Baraza hilo kwa niaba ya nchi zote 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya. Umoja wa Ulaya ambao hivi karibuni uliidhinisha rasmi mapendekezo yaliyomo kwenye mkataba wa Lisboni,una rais wake.