Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malengo ya milenia yanaweza kufikiwa Ulaya licha ya athari za uchumi:UNICE

Malengo ya milenia yanaweza kufikiwa Ulaya licha ya athari za uchumi:UNICE

Nchi kadhaa za Ulaya zinakabiliwa na kitisho cha kushindwa kufikia malengo ya maendeleo ya Mellenia licha kwamba nchi hizo zilikuwa zimepiga hatua kubwa katika siku za hivi karibuni.

Kwa mujibu wa report mpya iliyotolewa na timu ya wataalamu wa wakala wa Umoja wa Mataifa anayefuatilia maendeleo ya melengo ya mellenia kwa nchi za Ulaya na Asia UNECE,hali hiyo inaweza kuchangiwa na sababu kadhaa.

Report hiyo imetaja kuwa mdororo wa kiuchumi ulioshuhudiwa hivi karibuni katika mataifa mengi, umepunguza kasi kwa nchi nyingi barani Ulaya kuyafikia malengo ya maendeleo ya mellenia. Nchi hizo kwa sasa zinapitia katika kipindi cha machipuo mapya ya kiuchumi baada ya uchumi wake kuyumba kufuatia mdororo huo wa kiuchumi.

Report hiyo ambayo pia itapewa nafasi kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kujadilia maendeleo yaliyopigwa juu ya kufikiwa kwa malengo hayo ya mellenia, kuanzia hapo Septemba 20-22 imehimiza kufanyika kwa marekebisho ya haraka kwenye maeneo ya sera na uchumi ili malengo hayo ya mellenia yapewe msukumo mpya.