Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO inatoa mafuzo kwa askari wa zamani DR Congo

MONUSCO inatoa mafuzo kwa askari wa zamani DR Congo

Mpango wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kustawisha nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO umeanza kutoa mafunzo kwa askari jeshi waliokuwa katika makundi mbalimbali wakati wa uasi ili waweze kuingizwa kwenye jeshi la taifa la polisi.

MONUSCO inasema mafunzo hayo yatasaidia katika suala la kuimarisha usalama kwenye nchi hiyo inayokabiliwa na machafuko. Askari 1500 ndio wanaotarajiwa kupata mafunzo hayo kama anavyoarifu mwandishi Mmolewa Mseke Dide kutoka DRC.

(RIPOTI MSEKE DIDE)