Skip to main content

Usafi ni muhimu kwa waathirika wa mafuriko Pakistan:WASH

Usafi ni muhimu kwa waathirika wa mafuriko Pakistan:WASH

Mamilioni ya watu walioathirika na mafuriko nchini Pakistan sasa wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa usafi hasa kwenye maeneo yaliyoathirika sana ya Sindh na Punjab.

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la maji, usafi na afya WASH linalofanya kazi kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF Bill Fellows, usafi ni muhimu mara nne zaidi kuliko maji safi ya kunywa kwa kuwa unasaidia kuzuia maambukizi ya maradhi ya mlipuko. Maelezo zaidi na Jason Nyakundi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Maeneo yaliyokumbwa na mafuriko nchini Pakistan upatikanaji wa maji safi linatajwa kuwa tatizo kubwa lakini hata hivyo kwa sasa kupitia kwa shirika la WASH watu milioni 2.5 wanapata maji safi ya kunywa. Fellows anasema kuwa UNICEF kwa ushirikiano na serikali wanatoa elimu kuhusu usafi kwenye kwambi za waathiriwa wa mafuriko kama moja ya njia ya kuzisaidia jamii zilizoathirika kuelewa umihimu wa mazingira safi.

Anasema kuwa mafunzo hayo yanawamasisha waathiriwa kujenga vyoo akisema kuwa hadi sasa vyoo 2,723 vimejengwa vinavyotumiwa na karibu watu 40,000. Wafanyikazi wa sekta ya afya nchini Pakistan pia nao wanaendelea kuwapa waathiriwa elimu ya usafi kama moja ya juhudi za kuzuia magonjwa yanayosambazwa kupitia maji. Hadi sasa watu 750,000 wamepata elimu ya usafi.