Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwarejesha kwa nguvu watu wa jamii ya Roma si haki: Pillay

Kuwarejesha kwa nguvu watu wa jamii ya Roma si haki: Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa ameshutumu hatua za ufaransa za kuwarudisha nyumbani watu wa jamii ya Roma pamoja na ripoti za mpango wa Marekani wa kutaka kuwaua watu wanaoshukiwa kuwa magaidi akisema kuwa huku ni ni kuenda kinyume na haki ya kushi pamoja na sheria.

Akiongea kwenye mkutano wa 15 wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa hatua hizo za ufaransa ni sera zinazowalenga watu wa jamii ya Roma na hali ya umaskini inayowakumba. Pillay ametoa wito kwa nchi za ulaya kubuni sera ambazo hazitengi watu wa jamii ya Roma. Amesema kuwa harakati za kukabiliana na ugaidi hazistahili kukiuka haki za binadamu.

Bi Pillay anasema kuwa anatatizika na ripoti kuhusu mpango wa marekani wa kuwasaka na kuawaua watu wanaokisiwa kuwa magaidi akisema kuwa hatua hizo ni kiunyume na sheria za kimatiafa zinaolinda haki ya kuishi.