Skip to main content

Mkutano kufanyika UM kabla ya kura ya maoni Sudan:Ban

Mkutano kufanyika UM kabla ya kura ya maoni Sudan:Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameitisha mkutano muhimu kwenye makao makuu ya Umoja wa mataifa kujadili hali nchini Sudan wakati inapojindaa kwenye kura ya kuamua ikiwa eneo la kusini mwa nchi hiyo litakuwa nchi inayojisimamia.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York Ban amesema kuwa mkutano huo utaaandaliwa tarehe 24 mwei huu kando mwa mkutano mkuu wa baraza la Umoja wa mataifa. Ban amesema kuwa kuwa Umoja wa mataifa utahakikisha kuwa kura hilo imendaliwa kwa njia ya uwazi na kufanyika kwa amani.

Kura hiyo ni kati ya makubalino yaliyotiwa sahihi mwaka 2005 na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenye vilivyodumu kwa muda wa miongo miwili kati ya eneo la kaskazini na kusini mwa Sudan. Wenyeji wa kusini mwa sudan watapiga kura mnamo tarehe 9 mwezi Januari mwaka ujao kuamua ikiwa watajitenga na Sudan au wasalie kuwa nchi moja.