Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wato milioni 925 bado wanakabiliwa na njaa duniani:FAO

Wato milioni 925 bado wanakabiliwa na njaa duniani:FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO na shirika la mpango wa chakula duniani WFP leo wamesema idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani bado ni kubwa licha ya mafanikio ya karibuni yaliyopunguza idadi ya waathirika na kufikia chini ya bilioni moja.

Makadirio ya karibuni ya watu wanaokabiliwa na njaa iliyokithiri kote duniani ni milioni 925 ikiwa imepungua kwa watu milioni 98 kutoka idadi ya mwaka jana ambayo ilikuwa bilioni 1.23.

Mkurugenzi wa FAO Jacques Diouf amesema hata hivyo kwa mtoto mmoja kufa kila baada ya sekunde sita kutokana na lishe duni ni dhahiri kwamba njaa inasalia kuwa janga na kashfa kubwa duniani jambo ambalo halikubaliki.