Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matatizo ya kiuchumi yanahitaji ushirikiano:UNCTAD

Matatizo ya kiuchumi yanahitaji ushirikiano:UNCTAD

Wanauchumi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na biashara na maendeleo UNCTAD wameonya kuwa sera za serikali za mataifa yaliyoendelea za kujikwamua kutokana na uchumi mbaya wa dunia hivi sasa huenda zikaathiri maendeleo na suluhu ya ajira kote duniani.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Wanauchumi hao wanasema kuwa kushindwa kuambatanishwa kwa sera kati ya nchi zilizostawi na zile zinazounukia kichumi kunahatarisha tena kurejea kwa hali hiyo kwa mara nyingine. Hata hivyo nchi za afrika zinatajwa kutoathirika zaidi na hali mbaya ya uchumi iliyoikumba dunia kwa kuwa hazihusiki zaidi na masoko ya kimataifa sawia na nchi zingine zilizostawi huku uchumi wa bara la afrika ukitarajiwa kukua kwa silimia tano mwaka huu.

Wanauchumi hao wanasema kuwa pato la jumla la dunia lilipungua kwa asilimia mbili mwaka uliopita ikiwa asilimi kubwa zaidi tangu vita vikuu vya pili vya dunia lakini hata hivyo pato hilo linatarajiwa kuimarika kwa asilimia 3.5 mwaka huu.