Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Athari za mafuriko Pakistan bado ni mtihani:OCHA

Athari za mafuriko Pakistan bado ni mtihani:OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema eneo lililoathirika na mafuriko nchini Pakistan ni kubwa na mtihani unaowakabili katika kutoa usaidizi hawajawahi kuhushuhudia hapo kabla.

OCHA inasema watu milioni 21 wameathirika na wanahitaji msaada na wengi hawajui hatma yao. Bado wengi hawawezi kupata kila kinachohitajika kama maji safi ya kunywa, huduma za afya na hata malazi.

OCHA inasema ingawa juhudi kubwa zimefanyika lakini bado kuna changamoto inayoikabili nchi hi na fungu la fedha litakalohitajika kukidhi haja ya waathirika litakuwa kubwa sana.

Kwa mujibu wa msemaji wa Shirika la afya duniani WHO Paul Garwood maradhi ya mlipuko yanaendelea kuwa tishio kwa waathirika na wameshathibitisha visa vya kipindupindu.