Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wakimbizi waangaliwe kwa kina:Coomaraswamy

Watoto wakimbizi waangaliwe kwa kina:Coomaraswamy

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu katika suala la watoto kwenye migogoro ya kutumia silaha Radhika Coomaraswamy amesema mahitaji na matatizo ya watoto ambao ni wakimbizi wa ndani lazima yaangaliwe kwa kina na kuchukuliwa uzito.

Bi Coomaraswamy ameyasema hayo leo mjini Geneva akihutubia kikao cha 15 cha baraza la haki za binadamu. Amesisitiza kuwa ingawa watoto wengi wanakabiliwa na shida lakini hazifikii za watoto ambao ni wakimbizi wa ndani.

(CLIP COOMARASWAMY RADHIKA)

Bi Coomaraswamy ameongeza kuwa wanawake na watoto lazima walindwe na kila linalowezekana lazima lifanyike ili kutathimini hali halisi, akitoa mfano wa matukio ya ubakaji wa watu wengi hivi karibuni nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kuweka taratibu na mipango ya kuijulisha jumuiya ya kimataifa kuhusu vitendo kama hivyo ili kuhakikisha hatua muafa zinachukuliwa kushughulikia.

Ameongeza kuwa la muhimu zaidi ni kuhakikisha wakle waliotekeleza vitendo kama hivyo wanakabiliwa na mkono wa sheria, kwani bila kuwajibishwa hakuna haki na bila haki hakuna kizuizi.