Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aipongeza jumuiya ya Ulaya kuongoza mazungumzo ya Kosovo

Ban aipongeza jumuiya ya Ulaya kuongoza mazungumzo ya Kosovo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameungana na mataifa mengine wanachama wa umoja huo kukaribisha hatua za Jumuiya ya Ulaya za kuongoza mazungumzo kati ya Serbia na Kosovo baada ya kutangazwa kwa Kosovo kama taifa huru mwaka 2008.

 Juma lililopita wanachama wote 192 wa umoja wa mataifa waliikaribisha hatua hiyo ya Jumuiya ya Ulaya na kukubaliana na uamuzi uliotolea na mahakama ya haki ya kimataifa ICJ mwezi Julai wa uhuru wa Kosovo swala ambalo Serbia inalipinga.

Majaji kwenye mahakama ya ICJ walikubaliana kuwa uamuzi huo haukuenda kinyume na sheria za kimataifa na maamuzi ya baraza la usamala la umoja wa mataifa la mwaka 1999 baada ya kumalizika kwa vita nchini Kosovo au sheria zilizofuatwa na mwakilishi wa katibu mkuu kwa niaba ya ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Kosovo. Ban pia amesema kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa mchango wake kwa juhudi hizo na kushirikiana kwa karibu na Jumuiya ya Ulaya.