Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za pamoja zahitajika kutokomeza nyuklia:Amano

Juhudi za pamoja zahitajika kutokomeza nyuklia:Amano

Mkurugezni mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA Yukiya Amano leo amefungua mkutano wa bodi ya magava wa IAEA mjini Vienna Austria.

Katika hotuba yake bwana Amano amegusia masuala ya usalama wa nyuklia, kuweka bayana masuala ya nyuklia, ulinzi, hakikisho la kutosambaza nyuklia na masuala ya bajeti zinazohusiana na nyuklia. Kuhusu usalama wa nyuklia bwana Amano amesema juhudi za vyombo vya sheria vya kimataifa zimeongezeka katika kufuatilia usalama wa nyuklia.

Hata hivyo amesema ikiwa ni miaka mitano tangu kufanyiwa marekebisho mkataba wa ulinzi dhidi ya nyuklia hatua zinakwenda polepole. Bwana Amano amezungumzia baadhi ya nchi kutotoa ushirikiano kuhusu ukaguzi wa vinu na miatambo ya nyuklia ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya watu wa Korea DPRK na pia nchi kama Syria kutotekeleza matakwa na mkataba wa NTP. Kwa Upande wa Iran amesema imeendelea kukaidi masharti ya IAEA

(SAUTI YA YUKIYA AMANO)

Bwana Amano amesema anaamini IAEA ni lazima ifanye lolote liwezekanalo kusaidia upokonyaji wa silaha za nyuklia na kuziweka bayana, inapoombwa ni lazima isaidie kuanzishwa kwa maeneo huru bila nyukli, iendelee kuzuia uzalishaji wa nyuklia na iongeze mara mbili juhudi za kuyasaidia mataifa kufikia lengo la kuwa na dunia huru bila nyuklia.