Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama limelaani vikali shambulio la kigaidi Vladikavkaz, Urusi

Baraza la Usalama limelaani vikali shambulio la kigaidi Vladikavkaz, Urusi

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio la kigaidi liliotokea Vladikavkaz katika Serikali ya Shirikisho la Urusi tarehe 9 septemba mwaka huu na kusabisha vifo vya watu wengi na kujeruhi wengine.

Wajumbe hao wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamesisitiza nia yao ya kupambana na mifumo yote ya ugaidi kwa kuzingatia majukumu yao chini ya mikataba ya UM.