Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kunahitajika muongozo mpya ili kukabiliana na tatizo la taka zitokanazo na vifaa vya umeme:UM

Kunahitajika muongozo mpya ili kukabiliana na tatizo la taka zitokanazo na vifaa vya umeme:UM

Mkutano wa kimataifa kuhusu taka zitokanazo na vifaa vya umeme umeandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP mapema wiki hii mjini Nairobi Kenya.

Makampuni ya programu za kompyuta, makampuni ya kutengeneza simu na serikali ya Kenya wamekutana kwenye makao makuu ya UNEP ili kuandaa muongozo mpya wa jinsi ya kudhibiti taka hizo. Mwandishi wetu kutoka Nairobi Jason Nyakundi ametayarisha makala juu ya suala hilo. Ungana naye.