Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwepo kwa maji safi latajwa kuwa suala muhimu la malengo ya milenia kwenye mkutano wa Stockholm

Kuwepo kwa maji safi latajwa kuwa suala muhimu la malengo ya milenia kwenye mkutano wa Stockholm

Washiriki kwenye mkutano wa juma moja wa maji unaofanyika mjini Stockholm umetoa wito kwa mkutano mkuu kuhusu malengo ya milenia kujadili suala la upatikanaji wa maji safi ya kunywa, usafi wa mazingira na maji kwa wote.

Kulingana na ripoti ya Stockholm ni kuwa maji yanastahili kutambuliwa kuwa moja ya masuala muhimi yanayostahili kujadiliwa kwenye mkutano huo. Ripoti hiyo inasema kuwa maji ni nguzo muhimu ya kuafikiwa kwa malengo mengine ya milenia ikisema kuwa ukosefu wa maji unawafanya watu kuwa maskini na kuwanyima mamilioni ya watu hadhi zao hasa akina mama na wasichana. Mkutano wa Stockholm ni wa kila mwaka na unawaleta pamoja wataalamu 2500, watoa maamuzi, wafanyibiashara kutoka kote duniani ili kubadilishna mawazo na kutafuta suluhu.