Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wapongeza jumuiya ya Ulaya kwa kujaribu kuleta mapatano nchini Kosovo

Umoja wa Mataifa wapongeza jumuiya ya Ulaya kwa kujaribu kuleta mapatano nchini Kosovo

Nchi wanachama za Umoja wa mataifa zimeipongeza jumuiya ya Ulaya kwa kujitolea kwake kuanzisha majadiliono kati ya Serbia na Kosovo baada ya kutangazwa Kosovo kuwa nchi huru kutoka Serbia mwaka 2008.

Mahakama ya haki ya kimataifa ICJ ilitangaza kuwa uamuzi huo haukuenda kinyume na sheria za kimataifa baada ya kumalizika kwa vita nchini Kosovo au sheria zilizofuatwa na mwakilishi wa Katibu Mkuu kwa niaba ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kosovo. Hata hivyo waziri wa mambo ya kigeni wa Serbia Vuk Jeremic amesema kuwa nchi yake haitambui uhuru wa Kosovo.