Skip to main content

Kundi la mabalozi kwenye Umoja wa Mataifa lashutumu mpango wa kutaka kuchoma Koran

Kundi la mabalozi kwenye Umoja wa Mataifa lashutumu mpango wa kutaka kuchoma Koran

Kundi la mabalozi kwenye Umoja wa Mtaifa OIC limelaani vikali mpango wa kutaka kuchomwa kwa Koran uliotangazwa na kanisa moja kwenye jimbo la Florida nchini Marekani

Kundi hilo kwa mara nyingine limeridhirishwa na hatua za rais wa Marekani Barack Obama na waziri wa mambo ya kigeni Hillary Clinton za kulaani mpango huo wa kuchomwa kwa Koran. OIC limesema kuwa kuwa pingamizi zinazoendelea kuongezeka za kulaani mpango huo ni ishara tosho kuwa suala hilo halikubaliki kamwe na jamii nzima ya wamarekani isipokuwa watu wachache walio na mipango ya kuzua chuki.