Uchumi mbaya duniani wasababisha zaidi ya watu milioni 210 kukosa ajira

Uchumi mbaya duniani wasababisha zaidi ya watu milioni 210 kukosa ajira

Shirika la kazi ulimwenguni ILO linasema kuwa hali mbaya ya uchumi iliyopoa duniani kwa sasa imesababisha zaidi ya watu miloni 210 kukosa ajira ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya watu wasio na ajira kuwahi kushuhudiwa.

Kwenye Ujumbe wake kabla ya mkutano utakaoandaliwa mjini Oslo nchini Norway siku ya jumatatu, mkuu wa shiriKa la ILO Juan Somavia amesema kuwa tatizo la ukosefu wa ajira limekuwa kubwa zaidi.

"Mamilioni wanafanya kazi wakiwa maskini, akina mama na wanaume wengi wanafanya kazi za ziada wakati wanahitaji kazi za siku nzima. Wengine wengi wamepoteza matumani ya kutafuta ajira. Wanne kati ya wafanyikazi watano duniani hawana kinga ya kazi zao. Tuna vijana milioni 45 wanaojiunga na ajira kila mwaka".

Somavia amesema kuwa huku vijana milioni 45 wakipata ajira kila mwaka ulimwengu sasa unakabiliwa na changamoto kubwa katika siku za usoni. Amesema kuwa mkutano huo wa Jumatatu utajadili njia za kutatua suala hilo na kupata suluhu la kudumu.