Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Redio inayofadhiliwa na UM huko DRC OKAPI yatunikiwa tuzo la IPI

Redio inayofadhiliwa na UM huko DRC OKAPI yatunikiwa tuzo la IPI

Redio moja inayofanya shughuli zake katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa ufadhili wa Umoja wa Mataifa imefanikiwa kunyakua tuzo ambayo hutolewa na taasisi ya kimataifa ya uandishi wa habari IPI.

Redio OKAPI ambayo inatajwa kuwa na wasikilizaji wengi katika eneo la nchi zinazozungumza Kifaransa, ilianza kufanya kazi zake nchini Congo miaka 8 iliyopita kwa shabaya ya kuhimiza hali ya maelewano na uletaji wa amani. Licha ya kuendesha vipindi vyake kwa lugha tano, lakini sehemu kubwa ya vipindi vyake inarusha katika lugha ya Kifaransa.

Imefanikiwa kutunikiwa tuzo hiyo kutokana na mchango wake wa kuhimiza hali ya maelewano na kuarifu mambo kwa kuzingatia hali ya weledi na kuwasukuma wananchi kwenye ujenzi wa taifa lao baada ya kumalizika kipindi cha machafuko.