Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 10 UN-HABITAT nimepitia milima na mabonde na kujifunza mengi:Tibaijuka

Miaka 10 UN-HABITAT nimepitia milima na mabonde na kujifunza mengi:Tibaijuka

Dr Anna Tibaijuka mwanamke wa kwanza kuliongoza shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT, ameliaga shirika hilo baada ya kuliongoza kwa muongo mzima.

Bi Tibaijuka ambaye kitaaluma ni mwana uchumi aliteuliwa kushika wadhifha huo mwaka 2000 na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati huko Kofi Annan. Kwa miaka kumi Bi Tibaijuka anasema amepitia changamoto nyingi lakini anaondoka sasa kwenda kujiunga na uwanja wa siasa katika nchi anayotoka ya Tanzania akiwa kifua mbele, hasa kwa mafanikio aliyoyapata na kujifunza mengi.

Mwandishi wetu Jason Nyakundi alimtembelea Bi Tibaijuka nyumbani kwake Nairobi na kumkuta yuko katika harakati za kufungasha mizigo kwani tarehe 31 August ndio alisema kwaheri kwa Umoja wa Mataifa. Amezungumza naye kuhusu safari hiyo ya miaka 10 UN-HABITAT ungana nao.