Rais wa baraza la usalama alaani tishio la kutaka kuchoma nakala za Koran
Rais wa baraza la Umoja wa Mataifa Ali Treki ni kiongozi mwingine wa Umoja wa Mataifa kutoa sauti juu ya hofu ya tishio la kiongozi wa Kikristo wa Marekani kutaka kuchoma nakama za Koran .
Treki amelaani vikali tishio hilo akisema litachochea chuki na ubaguzi kati ya dini na imani na kuchagiza mgongano baina ya ustaarabu na dini duniani. Kanisa dogo lililoko Florida hapa Marekani liitwalo The Dove World Outreach center limearifiwa kusema litaendelea na nia yake ya kuchoma nakala za Koran kwenye siku ya kumbukumbu ya mashambulizi ya September 11 licha ya nia hiyo kulaaniwa vikali kote duniani.
Kauli ya Treki inafuta kama hizo ambazo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, na Mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA Staffan de Mistura. Viongozi mbalimbali wa dunia wamekuwa wakitoa tamko kuhusu tishio hilo na kusema litafungua mlango zaidi kwa ugaidi. Viongozi hao ni pamoja na Rais Barack Obama aliyesema kiongozi huyo wa dini anapaswa kufikia athari za kuamua kufanya kitengo kama hicho.
Mvutano huo umezusha hofu ya usama na leo shirika la polisi wa kimataifa INTERPOL limetoa tahadhari ya kimataifa kwa wanachama wake nchi 188 kufutia ombi la waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan, kwamba endapo kitendo hicho cha kuchoma Koran kitatekelezwa ,kuna uwezekano mkubwa wa kuzuka mashambulizi dhidi ya wasio na hatia.