Majadiliano ndio njia pekee kwa amani ya Israel na Palestina:Ban

Majadiliano ndio njia pekee kwa amani ya Israel na Palestina:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema majadiliano ndio njia pekee itakayowezesha Israel na Palestina kutatua tofauti zao.

Ban ameyasema hayo leo baada ya mkutano na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Mashariki ya kati seneta George Mitchel ambaye amemweleza katibu mkuu kuhusu mtazamo wa duru ya kwanza ya mazungumzo ya ana kwa ana baina ya Israel na Palestina. Bam amesema anatambua umuhimu na haja ya msaada wa jumuiya ya kimataifa katika mchakato huo wa amani ikiwa ni pamoja na jukumu la Umoja wa Mataifa na Quartet.

Ameongeza kuwa anatarajia kukutana na waziri mkuu wa Benyamini Netanyahu na Rais Mahamoud Abas wakati wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa baadaye mwezi huu. Amempongeza Rais Barak Obama wa Marekani, waziri wake wa mambo ya nje Hillary Clinton na seneta Mitchell kwa kufanya kazi bila kuchoka na kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika juhudi za amani ya Mashariki ya Kati.