Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

AMISOM, IGAD na UNPOS wamelaani shambulio dhidi ya AMISOM Somalia

AMISOM, IGAD na UNPOS wamelaani shambulio dhidi ya AMISOM Somalia

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Dr Augustine Mahiga, mwakilishi maalumu wa mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika kwa Somalia balozi Boubacar Diarra na mpatanishi wa IGAD kwa ajili ya amani na maridhiano ya kitaifa Somalia Kipruto arap Kirwa wamekuwa mjini Moghadishu kwa mazungumzo na Rais Sheikh Sharif Ahmed.

Wajumbe hao wamejadiliana na Rais Ahmed masuala muhimu yanayohusiana na mchakato wa amani nchini Somalia. Wakiwa Moghadishu leo wamefahamishwa kuhusu shambulio la kujitoa muhanga dhidi ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja muungano wa Afrika Somalia AMISOM. Katika shambulio hilo wanajeshi wawili wa AMISOM wameuawa, watu wamejuruhiwa vibaya na raia kadhaa wameuawa pia.

Wajumbe hao wamelaani vikali shambulio hilo luililotokea kwenye uwanja wa ndege wa Moghadishu siku ambayo ni mkesha wa sikukuu ya Eid-ul-Fitr ambayo ni ishara ya amani na upendo kwa Waislamu.

Wametoa pole kwa familia za waathirika, serikali ya Uganda na familia. Pia wamewataka Wasomali kupinga machafuko na kukumbatia amani.