Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mipango ya makazi mijini yapata tuzo ya UN-HABITAT

Mipango ya makazi mijini yapata tuzo ya UN-HABITAT

Idara zinazohusika na utoaji wa makaazi katika sehemu za mijini zimeibuka washindi wa tuzo la umoja wa mataifa kufuatia juhudi zao za kuwapa makao bora na maenedeleo ya mijini wakaazi wake .

 Nchini China manispaa ya mji wa Kunshan pia nao utapokea tuzo hilo kwa kuwapa wanyeji wake huduma muhimu. Mjini huo pia umetajwa kuwavutia watafuta ajira 800,000. Usimamizi wa mji huo pia umewahakikisha kuwa wakaazi wake wamejumuishwa kwenye mpango wa malipo ya uzeeni , matibabu , usawa wa kupata elimu na pia kuhakikisha kuwa wenyeji wake wamepata huduma sawa za umma.