Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umetoa wito wa ushirikiano zaidi wa kimataifa na majadiliano kukabiliana na ugaidi

UM umetoa wito wa ushirikiano zaidi wa kimataifa na majadiliano kukabiliana na ugaidi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka kuwepo na ushirikiano wenye nguvu baina ya Umoja wa Mataifa,serikali, mashirika ya kikanda na jumuiya za kijamii katika juhudi za kutekeleza mikakati ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na ugaidi.

Ban amesema kwa kufanya hivyo watafanikiwa kutokomeza tishio na kukumbatia amani na usalama wa kimataifa. Maelezo zaidi na Jason Nyakundi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

"Kwenye ripoti yake kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa Ban ameridhika na kazi inayofanywa na umoja wa mataifa kupambana na ugaidi akioneza kuwa hata hivyo umoja wa mataifa inahitaji kufahamu kwa kina mbinu za kupambana na ugaidi ili kuchukua hatua zifaazo kwenye ngazi za chini na zile za kimataifa.

Mwaka 2008 baraza la usalama la umoja wa mataifa lilitoa wito kwa nchi wanachama na mashirika mengine duniani kuweka mikakati ya kutekeleza makubalioo hayo kwa pamoja yalibonuniwa na umoja wa mataifa mwaka 2006 na yanayotoa mwelekeo wa jamii ya kimataifa kuhusu njia za kukabiliana na ugaidi."